Haya ndiyo maeneo ambayo fainali ya Croatia vs Ufaransa itaamuliwa

 

 Baaada ya safari ya karibia mwezi mzima hatimaye siku ya Jumapili tutashuhudia fainali ya kombe la dunia kati ya Ufaransa dhidi ya Croatia, kabla ya mchezo huo ni vyema tukaangalia maeneo ambayo mechi hii inaweza kuamuliwa.

 1. Mashambulio ya pembeni.

 Hadi sasa kufika fainali ya kombe la dunia timu za Croatia na Ufaransa zimekuwa na madhara zaidi katika beki ya kulia, Croatia wameshashambulia kwa 45% kutokea upande wao wa kulia, huku kushoto ikiwa 33%, Ufaransa wenyewe wameshambulia kwa 42% kutoka kulia na 37% kushoto.

 Sime Vrsaljokos amekuwa mzuri sana katika kupanda mbele na kupiga kross kwa upande wa kulia wa Croatia na moja ya kross zake ndizo zilizaa bao la kusawazisha la Perisic vs Uingereza lakini pia tuliona namna ambavyo Ashley Young na Trippier iliwabidi kukaa nyuma baada ya Perisic na Rebic kuwasha motoo.



 Wafaransa nao kama ilivyo kwa Croatia, Benjamin Pavard amekuwa kati ya walinzi bora kabisa wa upande wa kulia msimu huu wa kombe la dunia na alifunga bao dhidi ya Argentina na upande huu wa Pavard ndiko Mbappe anakotokea.



 Wakati Mbappe na Pavard wakiwa wanapush upande huu wa kulia, kushoto yupo Lucas Hernandez na Blaise Matuidi ambao mara zote wameonekana wakipambana kukokota mipira kwenda mbele na kujaribu kuipiga kros lato kati.

 2. Kylian Mbappe.

 Hii inaweza kuwa hukumu ya mechi hii ya fainali, sahau alivyowaua Argentina lakino katika mecho dhidi ya Uingereza dakika ya 1 tu alikimbia na mpira ambao almanusra Ufaransa wapate bao la kuongoza.

 Dejan Lovren na Damagoj Vida hawako vizuri kumkaba mchezaji kariba ya Mbappe, lakini mlinzi wa kushoto wa Croatia Ivan Strinic naye anaonekana hana kasi sana na hapa ndio wasiwasi unapokuja namna ambavyo Croatia watamzuoa Mbappe.

 

Namna bora kwa Croatia kumzuia Mbappe ilikuwa ni msaada kutoka winga wa kushoto lakini kushoto kwa Croatia yuko Ivan Perisic ambaye anakuwa bora timu ikiwa na mpira tu na hii inaweza kumpa space Mbappe kuwakimbiza Wacroatia upande huu wa kushoto.

 3.Pogba/Kante vs Ractic/Modric. 

Hapa ndipo mafundi mitambo wa mchezo huu walipo, na hapa mwenye akili kuliko mwenzake ndiye ambaye ataamua namna mchezo huu utamalizika na ndipo mipango yote ya fainali hii inaanzia.

 

 Paul Pogba amekuwa mtamu sana safari hii amekuwa akiichezesha sana Ufaransa lakini hii inachagizwa na ulinzi imara alionao kutoka kwa Ngolo Kante na ulinzi wa Matuidi katika flank ya kulia na hii imemfanya Pogba kuwa huru sana.

 

 Lakini tunamuona Pogba kama kiungo bora ila amekutana na Modric na Ractic? Modric amekuwa kama mchawi katika kombe la dunia, namna pasi zake anavyopiga amekuwa kama mtu anaeamuru mpira utoke sehemu moja na kwenda pengine na mpira unatii.

 Hadi sasa Modric amekimbia kilomita nyingi kuliko mchezaji mwingine kombe la dunia 63, hakuna mchezaji Croatia aliyemzidi kwa mabao, ametengenexa nafasi nyingi na ukimsimamisha Modric baasi umeizima Croatia lakini unamsimamishaje huku Ractoc yupo pembeni? Na hapo ndipo Pogba na Kante inabido wakune vichwa.

 4. “Super Mario” Mandzukic.

 Hakuna mtu aliyeko salama pale Mandzukic anapokuwa katika 18, achana na kutozionea aibu nyavu lakini ni kariba ya mshambuliaji mwenye spirit ya ushindi, mda wote unamuona ni mtu anayetafuta kitu uwanjani.

 Mchezo dhidi ya Uingereza kwa mfano, alionekana kuwanyima raha sana kina John Stones pamoja na wenzake na baada ya kupoteza comfortability Stones alipoteza mpira ambao Mandzukic aliiba na kufunga bao lililowaondoa Uingereza.

 

Raphael Varane atakuwa katika wakati mgumu na Mandzukic, hadi sasa mshambuliaji huyu wa Juventus ameshashinda mipira ya hewani kwa 72% na rekodi hii inamuweka mashakani mlinzi yeyote anayecheza dhidi yake, na hili linakuwa jambo lingine la kuamua ushindi wa Ufaransa na Croatia.

Comments

Popular posts from this blog

Official : Simba sign Lusaka dynamos captain

CECAFA Cup final: Kagere starts for Simba as Azam looks to defend title

Barcelona yaongeza dau la willian